Best Poem of Fadhy Mtanga

Ada Ya Mja
Hili linawezekana, ijapokuwa ni gumu,
Na halitoshindikana, ndiyo yetu majukumu,
Nitakufundisha sana, mi hapa ndiyo mwalimu.

Mimi sishindwi na kitu, sijawahi asilani,
Ncha yangu siyo butu, ina makali fulani,
Mimi ni mtu wa watu, tangia hapo zamani.

Kila kitu ninaweza, hakuna nisichojua,
Read the full of Ada Ya Mja
Nakupa Wewe Zawadi
Nimekaa nikawaza, nini unastahili,
Jambo lenye kupendeza, jambo lenye kuhawili,
Vema lenye kueleza, kwazo hisia kamili,
Nakupa wewe zawadi, nayo ni pendo la dhati.

Kila nachofikiria, bado siwezi ridhika,
Kiwezacho kufikia, mapenzi yalotukuka,
Mola alokujalia, yale yasomithilika,
Nakupa wewe . . .
Read the full of Nakupa Wewe Zawadi